INAPASWA AKUBARIKI KABLA HAJAFA

| Video

SIKU 10 ZA SEPTEMBER TO REMEMBER:
            {PRAYER POINTS ZA USIKU} 
                   DAY 02:Sept 24,2025
INAPASWA AKUBARIKI KABLA HAJAFA

Mwanzo 27:4 
Uniandalie chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili nikubariki kabla sijafa.”

Kati ya kundi ambalo hatupaswi kabisa kulisahau kwenye ratiba za maombi ya kila siku katika jamii na familia zetu,ni watu wazima,wale watu ambao umri wao ni mkubwa kutuzidi wengine ndani ya familia,au tunaweza kuwaita wazee.

Nifuatilie hapa nikusaidie kitu, unaweza kuwa na sababu zote za kuwalaumu,labda kwa sababu hawakusimama kwenye nafasi zao kwa sababu mbalimbali,na mmejikuta mnapitia mazingira sio mepesi sana na unawatupia lawama…ni sawa….ila kabla ya kulaumu chochote kuhusu wao,unatakiwa kuelewa kuwa pamoja na mambo yote maovu au mabaya waliyoyatenda kwa kudhamiria au kuto kudhamiria,ila nafasi zao Mungu anaziheshimu na zinabaki palepale na thamani zao ndani ya familia na jamii.

Uwepo wao ndio unaendelea kuunganisha familia kwenye umoja,upendo na mshikamano. Leo unaweza kuwachukulia poa ila siku ambapo hautakuwa na uwezo wa kuwaona tena mbele ya macho yako ndipo utagundua kuwa walikuwa na maana sana kuwepo,hata kama ni masikini, hawajasoma,hawana cha kukusaidia….ila Mungu amewaweka hapo kwa makusudi maalu.

Leo tunawaombea hao tu, hakikisha unafanya maombi kwa mzigo sana,kama ni mzazi wako au mlezi wako nk, muombee kwa Mungu mambo makubwa mawili
Umri wake ukawe timilifu na asiondoke kabla ya wakati
Hekima ya kusimama katika nafasi yake ndani ya familia.

Familia nyingi leo hii zimegawanyika na kila mtu anaishi kivyake kwa sababu ya kukosekana kwa mtu mzima ambaye atakuwa pale nyumbani tu.

Usiache kuwakumbuka kwa matunzo, watunze,walishe na kuwavika kwa kadiri unavyojaliwa na Mungu, angalia hili andiko hapa katika kitabu cha 1 Timotheo 5:8 
Lakini mtu yeyote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Hawa watu ni baraka sana katikati yetu, na usisubiri uwapoteze au umpoteze ndipo ugundue hili mtu wa Mungu.
Mithali 16:31
Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki.

Tuamke usiku leo saa TISA na tutakuwa na maombi maalum kwa ajili yao, Youtube channel ya SIRI ZA BIBLIA

Pastor Innocent Mashauri
Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA
Maarifa ya ki-Mungu
+255 758 708804


 SADAKA